JESHI
la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawashikilia
watu 10 kwa udhalilishaji wa kumchapa viboko mwanamke hadharani.
Watu
hao ni wa kijiji cha Kinesi tarafa ya Suba wilayani Rorya. Miongoni mwa
watu hao, wamo viongozi watano wa baraza la mila liitwalo Irienyi ndogo
la kabila la Wasimbiti.
Watu hao wanatuhumiwa kumchapa viboko zaidi ya 30 hadharani mwanamke huyo, kitendo kilichomdhalilisha mbele ya jamii.
Mapema
wiki hii, baadhi ya video ilisambaa katika mitandao ya kijamii,
ikimuonesha mwanamke akichapwa viboko na wanaume kwa zamu huku akilia
mbele ya hadhara na sauti za wanaume zilisikika zikishabikia kitendo
hicho.
Kamanda
wa Polisi Tarime/ Rorya, Andrew Satta alisema kuwa tukio hilo ni la
Desemba 23 mwaka jana mchana katika kitongoji cha Migutu kijiji cha
Kinesi tarafa hiyo ya Suba wilayani Rorya katika maeneo ya Mastooni,
ambako kulikuwa na mkutano wa Ritongo wa mila.
Mwanamke
huyo mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa kijiji hicho (jina
limehifadhiwa) aliitwa na kufuatwa na vijana na kupelekwa katika mkutano
huo wa mila, uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa kijiji hicho. Ilidaiwa
kuwa mwanamke huyo alimtuhumu mama yake mzazi wa umri wa miaka 55 kuwa
ni mchawi.
Kwamba hamtambui na kumkana kuwa si mama yake mzazi; huku akidai kuwa mama huyo anataka kumuua kwa uchawi.
Kamanda
Satta alisema katika mkutano huo wa baraza la mila la Irienyi, vijana
sita waliamriwa kumchapa kila mmoja viboko vitano makalioni mwanamke
huyo, hali iliyomsababishia majeraha, kumuathiri, kumdhalilisha na
kumshushia utu wake kwa jamii.
****
No comments:
Post a Comment